Thursday, 19 October 2017

JE WAFAHAMU MADHARA YA KUMBEMENDA MTOTO?











Dhana hii iliyoonea maeneo ya Pwani hususan mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Lindi, Tanga na Morogoro inaelezwa kuwa inatokana na wazazi wa mtoto kujihusisha na mapenzi pindi anapokuwa bado mchanga.

Kumbemenda mtoto ni mtoto kutokua vizuri ikidhaniwa kutokea kutokana na mama anayenyonyesha mtoto kukutana kimapenzi na mwenzi wake hasa kipindi mtoto bado ni mchanga na ananyonyeshwa.


Hii ni dhana iliyopo katika jamii mbalimbali, na inadhaniwa hutokea kwa sababu mtoto kunyonya maziwa yenye mbegu za kiume zilizoingia kwenye maziwa baada ya kufanya mapenzi.

Je, kuna ukweli wowote?
Hapana. kiukweli na kiutaalamu dhana hii si sahihi kabisa!
kufanya mapenzi na mwenzi wako baada ya kujifungua hakuwezi kusababisha afya ya mtoto kuzorota. mwanamke anapokutana na mwanaume kimapenzi, shahawa huingia kwenye tumbo la uzazi na kubaki huko. haziingii kwenye damu wala haziwezi kufika kwenye maziwa. dhana ya kuwa shahawa huingia kwenye maziwa na kumuathiri mtoto sio sahihi.

Ni baada ya muda gani mwanamke aliyejifungua anaweza kufanya mapenzi?
unaweza kuanza kufanya mapenzi tena baada ya maji maji yenye damu ya uke (lochia) kuacha kutoka ambayo ni kama wiki 3 mpaka 4 baada ya kujifungua, na wewe kujisikia vizuri na kuwa tayari kushiriki katika mapenzi. pia, mnaweza kusubiri mpaka wiki 6 zipite toka ulivyojifungua.

Je, kuna athari yoyote ya kufanya mapenzi baada ya kujifungua?
Kufanya mapenzi baada ya kujifungua hakuwezi kuleta madhara kwa mtoto endapo hamna maambukizi ya magonjwa kama virusi vya ukimwi (vvu). ikiwa mwanaume ana vvu anaweza kumuambukiza mama na kisha mtoto kuambukizwa kupitia maziwa ya mama.

Ikiwa mnafanya mapenzi kabla ya damu damu ya ukeni kukata, maambukizi ya bakteria yanaweza kutokea kwenye tumbo la uzazi (endometritis). pia kuna uwezekano wa mama kupata ujauzito miezi 6 ya kwanza ya kunyonyesha.

Nini kinasababisha afya ya mtoto kuzorota?
Kama tulivyoona, kufanya mapenzi hakusababishi mtoto kubemendwa. afya ya mtoto inaweza kuzorota kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo;

  • Kukosa maziwa ya mama ya kutosha
  • Mtoto kushindwa kunyonya vizuri
  • Kuanzishiwa vyakula vya ziada mapema, kabla mtoto hajafikisha miezi 6 au vyakula visivyo na viritubisho vya kutosha.
  • Homa, nimonia na maambukizi ya mfumo wa mkojo (uti) za mara kwa mara.
  • Maambukizi ya magonjwa kama virusi vya ukimwi (vvu) au kifua kikuu.
  • Matatizo ya moyo ya kuzaliwa nayo (congenital heart diseases).

Kufanya mapenzi na mwenzi wako hakusababishi mtoto kubemendwa. baada ya kujifungua mtoto hutegemea kupata lishe bora kutoka kwenye maziwa ya mama, hivyo nyonyesha mtoto wako vizuri. ukiona ukuaji wake unazorota, onana na daktar

No comments:

BLOG LIST