Serikali imesema kuwa katika mwezi huu, mishahara ya watumishi wa umma itaongezwa baada ya kukaa muda mrefu, kutokana na zoezi la uhakiki wa watumishi lililokuwa likiendelea.
Hayo yamesemwa na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi, leo Jumapili, Novemba 5, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiiana na tathmini ya miaka miwili ya miaka Rais Dkt. John Pombe Magufuli madarakani tokea alipoapishwa, Novemba 5, 2015.
“Mwezi huu mishahara ya wafanyakazi wa Serikali itaongezwa kama Rais Magufuli alivyoahidi” alisema Dkt. Hassan Abbasi.
katika tathmini hiyo msemaji mkuu wa serikali alieleza kuwa serikali imeweza kuokoa sh. 236 bilioni kutokana na uhakiki wa watumishi hewa zaidi ya 20,000 na sh. 149 bilioni kutokana na uhakiki wa watumishi wenye vyeti feki.
Dkt. Abbasi amewashukuru wananchi kwa kuonyesha kijitoa pamoja na kunga mkono juhudi za kuleta maendeleo kwa nchi ya Tanzania zinazofanywa na serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa Rais John. pombe Magufuli.
No comments:
Post a Comment